KATIKA hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amenaswa akiwa ametinga khanga moja na kuwaacha watu midomo wazi.
Kajala alinaswa na kamera yetu maeneo ya Kigogo jijini Dar ambapo watu kibao walionekana kumzunguka na kuhoji kulikoni staa huyo ambaye amezoeleka kutika pamba kali, aonekane na vazi la khanga?
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Kajala alisema alilazimika kutinga khanga hiyo kuendana na matakwa ya filamu yaliyomtaka kuvaa vazi hilo na kuonesha mazingira ya uswahilini hivyo watu waliomzunguka walikuwa hawajui nini kinaendelea.
“Nilipoambia naigiza sinema ya Kigodoro nilishtuka sana lakini mwisho wa siku nilikubali kwa kuwa mimi ni msanii naweza kubadilika kivyovyote na nina imani mashabiki wangu wataniona kivingine, humo ni full mcharuko,” alisema Kajala.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo December 29, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania December 29,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetin...
3 hours ago
0 comments:
Post a Comment