Tuesday, August 12, 2014

Thursday, October 24, 2013

IMEVUJA! Kumbe ile safari ya nchini China ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ lengo lilikuwa kubadili ngozi ya mwili wake katika mwonekano mpya ambayo ilishaharibika kwa mkorogo, Amani limetonywa.
Wema Sepetu ‘Madam’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, staa huyo aliingia nchini humo na mdogo wake aitwaye Bite ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kufanya mawasiliano na nyumbani, Tanzania endapo lingetokea baya wakati wa zoezi hilo.

KWA NINI ALIAMUA KUDILI NA NGOZI?
Mpashaji wetu aliliambia Amani kwamba, Wema alichoshwa na ‘vijembe’ vya watu mbalimbali wakiwemo wabaya wake kuwa ngozi yake imebabuka kwa kutumia mkorogo kupitiliza.
Miguu ya Wema Sepetu ‘Madam’ kabla ya kubadili ngozi.

“Kuna wakati Wema alikuwa akikosa amani kutokana na maneno ya watu, wengine waliokuwa wakimrushia vijembe ni masupastaa wenzake, ndiyo maana akaamua kwenda China kubadili ngozi yake iwe na mwonekano mpya,” kilisema chanzo.

Habari zaidi zilidai kwamba, supastaa huyo hakupenda kabisa Wabongo wajue kuwa yupo China kubadili ngozi, hata baadhi ya magazeti yalipoandika amekwenda kujirusha na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alimshukuru Mungu siri yake imesitirika.
Wema.

UBADILISHAJI WA NGOZI WATUMIA SAA 12
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Wema aliingia kwenye kliniki ya ngozi katikati ya mwezi Oktoba, saa 3:12 asubuhi na shughuli ikamalizika saa 2:25 usiku.
“Alikaa kliniki toka saa tatu na dakika kumi na mbili asubuhi hadi saa mbili na dakika ishirini na tano usiku,” kilisema chanzo.

MADAKTARI WAMWONYA
Habari zaidi zinaeleza kuwa, madaktari waliokuwa wakimfanyia zoezi hilo walipomaliza walimuonya kutorudia tena kutumia mikorogo au aina yoyote ya losheni zenye kubabua ngozi, kama vile carolite.

SEHEMU ZILIZOHARIBIKA SANA
Kwenye mwili wa Wema, sehemu zenye mikunjo kama nyuma ya magoti, kukaribia makwapa, mapajani na mbele ya viwiko ndizo ziliongoza kwa kuharibika hali iliyokuwa ikimfanya mara nyingi ashindwe kuvaa sketi za vimini.

SHILINGI MILIONI 13 ZAYEYUKA
Katika zoezi hilo, Wema ambaye pia ni msanii wa filamu za Bongo na bosi wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame Production ya jijini Dar, ametumia shilingi za Tanzania, milioni 13 ikiwa ni pamoja na nauli yake na Bite kwenda China na kurudi, malazi na chakula.

APEWA DAWA YA KUZUIA KUZEEKA MAPEMA
Baada ya ubadilishaji huo wa ngozi, Wema alipewa dawa ambazo zitamsaidia kutozeeka mapema.
AONYWA MATUMIZI YA SIGARA NA KUTOLALA KWA WAKATI
Mbali na dawa hizo, staa huyo alionywa na matumizi ya sigara aina yoyote ile na kujipanga upya kwenye suala la kulala mapema ili apate usingizi wa kutosha.

MENEJA WAKE ATINGA CHINA KUHAKIKI NGOZI
Habari zaidi zikawekwa wazi kwamba, Wema alimwita meneja wake, Martin Kadinda kwa lengo la kuhakiki mwonekano mpya wa ngozi ya staa huyo.

Juzi, Amani lilimtafuta Dk. George wa zahanati maarufu ya Sino iliyopo Sinza Mapambano (Kwawachina) ambapo alisema warembo wengi hubadili ngozi kwa mtindo wa plastic surgery, mara nyingi sehemu yenye mikunjo au kuharibika hukatwa na kuvutwa, kama mtu alishaanza kuzeeka huonekana kijana.

“Nchi maarufu kwa kubadili ngozi ni Thailand, lakini China na Afrika Kusini zimeanza kutoa huduma hiyo.
“Hapa nchini bingwa wa masuala ya ngozi ni Profesa Masawe, zamani alikuwa Muhimbili kwa sasa ana kituo chake upanga Dar,” alisema Dk. George.

Kuhusu madhara, Dk. George alisema hayako wazi sana inategemea maisha ya mtu ya kila sikiu.

MENEJA WA WEMA AZUNGUMZA
Baada ya gazeti hili kuzinyaka habari hizo, lilimtafuta meneja wa Wema, Martin Kadinda alipoulizwa alikiri kwenda China kwa ajili ya kuhakiki mwonekano mpya wa ngozi ya ‘Beautiful Onyinye’ huyo na kusema kuwa ilikuwa lazima bosi wake afanyiwe hivyo kwa sababu bosi ni kioo cha jamii.

“Unajua Wema ni kioo cha jamii, hivyo si vyema watu kumsema kwa kitu kidogo kuhusu ngozi yake kwani hata yeye alikuwa hapendezwi nayo. Lakini nashukuru sana kwa sasa ana mwonekano mpya wa ngozi.

“Nilikwenda kuhakikisha kama ngozi yake kwa sasa inaweza kuwa na mwonekano mpya, ni kweli wamefanikiwa madaktari. Wamempa masharti kadhaa, kama kulala sana, lakini pia wamempa dawa nyingine,” alisema Kadinda.

WEMA MWENYEWE SASA
Baada ya kuzungumza na Kadinda, Amani lilimuendea hewani Wema ili kumsikia na yeye kuhusu kubadili ngozi nchini China.
Amani: Mambo Wema, za China?
Wema: Salama tu, niambie.

Amani: Hapa kuna habari kuwa safari yako ya China ilikuwa kwa ajili ya matengenezo ya ngozi yako, vipi ni habari za kweli?
Wema: Ah! Sasa ngozi yangu imekuaje kwani?
Amani: Inasemekana una mwonekako mpya wa ngozi, ile ya kwanza hukuipenda kwa sababu ya kujeruhiwa na mkorogo.
Wema: (kimya kidogo) oke, sikupenda kulizungumzia hilo kwa sasa lakini ndiyo hivyo kama ulivyosikia.

Amani: Unaweza kuniambia ni shilingi ngapi umetumia?
Wema: Mh! Mbona unanikaba koo jamani? Kama shilingi milioni 13 pamoja na gharama za usafiri.
Amani: Nashukuru sana Wema.
Wema: Karibu sana.
Diamond akiwa katika Viwanja vya Leaders jana
..Akingololoka kidogo viwanjani hapo.

MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma yake ya 'Number One', Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' baada ya kutua jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini China, alitembelea katika Viwanja vya Leaders ambapo maandalizi ya shoo ya Fiesta 2013 yanafanyika.

Akiwa viwanjani hapo, Diamond aliwataka mashabiki wake wote kuhudhuria shoo hiyo itakayofanyika siku ya Jumamosi Oktoba 26 mwaka huu. Kupitia akaunti yake ya Instagram na tovuti yake, msanii huyo aliandika yafuatayo:

" Kwa heshima ya mashabiki wangu, nchi na taifa langu, ilinibidi nirudi maalumu kabisa kwa ajili ya shoo hii ya Fiesta Jumamosi pale Leaders Club ili kuwakaribisha wageni zetu kutoka nje. Lakini pia kuwadhihirishia wageni hao kuwa Tanzania si legelege imebarikiwa wasanii na wenye uwezo...! Tukutane pale Leaders on Saturday Mdau wangu..." aliandika msanii huyo.

Saturday, October 19, 2013

STAA wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amekiri kuwa huwa anatumia sigara ‘fegi’ ili kuondoa mawazo.
Wema alifunguka hayo juzikati kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa na Runinga ya East Africa ambapo alikuwa akifungukia maisha yake likiwemo suala hilo la kuvuta sigara.
“Huwa navuta sigara pindi ninapokuwa na mawazo, nikivuta huwa inanisaidia kupunguza na kunifanya niwe vizuri,” alisema Wema.
STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kujihusisha na masuala ya muziki, isipokuwa aliingia katika fani hiyo kwa kufuata mkumbo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nisha alisema imekuwa ni aibu kubwa kujikita kwenye fani hiyo na kukaa kimya kwa kipindi kirefu kwa kuwa hana mapenzi ya dhati na fani hiyo kama ilivyo kwenye filamu.
“Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu,” alisema Nisha.
MAISHA ya Anthery Andreas Mushi (40) anayedaiwa kumpiga risasi mzazi mwenzie, Ufoo Peter Saro, kumuua kwa risasi mama wa Ufoo kisha kujiua yeye mwenyewe, yameanikwa, Risasi Jumamosi inayadadavua.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ambaye aliomba asiandikwe jina gazetini kwa sababu hakuwa msemaji wa familia, maisha ya Anthery akiwa Sudan kikazi yalikuwa ya kujinyima sana.
Alisema marehemu aliishi hivyo kwa lengo la kuhifadhi sehemu kubwa ya mshahara wake ili aweze kujijenga kimaisha kwa kuwa mpango wa kufunga ndoa na Ufoo ulikuwa upo.

ALIKUWA AKILA MARA MBILI KWA SIKU
Ndugu huyo alisema marehemu alikuwa akila mara mbili tu kwa siku yenye saa ishirini na nne, asubuhi ya saa tatu na usiku wa saa moja.
“Jamaa aliishi maisha ya kujinyima sana. Lengo lake lilikuwa kujiwekea akiba ya fedha za mshahara ili aweze kutengeneza maisha huku Dar.
“Mwaka jana alinitumia dola za Kimarekani elfu kumi (sawa na shilingi Mil. 16 za Tanzania) nimuwekee, lakini baadaye akaniambia nimrudishie ili amtumie mtu ambaye atampa maagizo ya ujenzi wa nyumba lakini hakuniambia ni nani wala nyumba inajengwa wapi,” alisema ndugu huyo.

HAKUWA NA MWANAMKE SUDAN
Ndugu huyo alizidi kusema kuwa marehemu hakuwa na mwanamke aliyekuwa akiishi naye Sudan kwa vile akili yake yote ilikuwa kwa Ufoo na alipanga baada ya kufunga ndoa angemfanyia uhamisho mkewe ili wakaishi wote nchini humo.
NDUGU WALISHAANZA KUONA MBELE JUU YA MAISHA YAKE
Habari zaidi zinadai kuwa, miezi ya karibuni alipenda kuwapigia simu baadhi ya nduguze na kuwapa malalamiko kuhusu uhusiano wake na Ufoo.
“Miezi ya karibuni alikuwa akitupigia simu baadhi ya ndugu na kulalamika kuwa kuna watu hapa Tanzania wamekuwa wakimtonya kwamba, wanasikia Ufoo anataka kuolewa na mwanaume mwingine.
“Tulimshauri kupuuza maneno ya watu kwa vile Ufoo mwenyewe hajamuwekea wazi au kama anaamini hayo maneno basi afadhali aachane naye kwa vile anaishi mbali, atakuwa akisikia maneno mengi kuhusu mzazi mwenzie huyo ambayo yatamuumiza.
“Lakini kuna siku alinipigia simu na kuniambia amefikia hatua ya kuchukua uamuzi mgumu kama mwanaume. Mimi nikajua labda atamuacha mzazi mwenzie, nilivyosikia hili la risasi nilishangaa sana,” alisema ndugu huyo.

MAITI YADAIWA KUTENGWA NA KANISA
Habari kutoka Uru Mawela, Moshi Vijijini zinasema kuwa, Kanisa la Roman Katoliki limeutenga mwili wa marehemu Anthery kwa sababu alizaa nje ya ndoa. Marehemu ana mtoto mmoja aliyemzaa na Ufoo, anaitwa Alvin Anthery Mushi (10).
Ikadaiwa kwa sababu hiyo, mazishi yake yaliyotarajiwa kufanyika jana Machame, Moshi yasingekuwa na ibada au misa ya kumwombea marehemu.

UFOO ALIMTUMA BOSI WAKE AKAMUAGIE MWILI WA MAMA YAKE
Kutoka Kibamba wakati wa kuuaga mwili wa mama wa Ufoo, Anastazia Saro, Mkurugenzi wa ITV na Radio One ambako Ufoo anafanyia kazi, Joyce Mhaville alisema alitumwa na mfanyakazi wake huyo kwenda kumwagia mwili wa marehemu kwa kuwa yeye asingeweza kufika.
Joyce aliyasema hayo Jumanne iliyopita wakati akisoma hotuba fupi kwa niaba ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Abraham Mengi.
MTOTO WA MAREHEMU AWALIZA WENGI
Katika mazishi ya mama Ufoo yaliyofanyika Uru Moshi, Jumatano iliyopita, mtoto wa Ufoo, Alvin aliwaliza wengi kutokana na mazito yaliyowapata wazazi wake.
KUNA simulizi ya majonzi nyuma ya kifo cha mwanamke Lewina Kinemo (38) aliyedaiwa kujirusha ghorofani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam ambako alikwenda kujifungua, Risasi Jumamosi lina mkasa mzima.
Lewina alifariki dunia Jumanne iliyopita saa tano na dakika arobaini alipokuwa anatoka kumnyonyesha mwanaye aliyezaliwa wiki moja nyuma.

MWANAMKE ALIYEKUWA NA MAREHEMU
Kwa mujibu wa mwanamke aliyekuwa na Lewina (jina halikupatikana mara moja) muda mfupi kabla ya kifo, marehemu alifanya mambo yenye viashiria vya kifo chake na hajui nini kilimtokea.
Alisema: “Unajua baada ya kujifungua, watoto waliopatikana na matatizo walitengwa kwenye chumba maalum ghorofa ya pili, sisi wazazi tukawa chini.
“Sasa tulikuwa tunatakiwa kupanda ghorofani kwenda kuwanyonyesha watoto kila baada ya saa tatu kupita. Ili kwenda, ililazimika kupanda lifti lakini kwa sababu yeye alijifungua kwa upasuaji, daktari alimshauri asiwe anapanda lifti.
“Tulipanda mara kadhaa, lakini safari ya mwisho ambayo marehemu alikutana na kifo chake, baada ya kumaliza kumnyonyesha mwanaye, alimshika akamwangalia sana kisha akasema maskini mwanangu sijui utabaki na nani?
“Mimi sikutilia maanani kauli yake, kumbe alijua atakufa.
“Kuna wakati tukiwa wodini alisema yeye ana duka la kushona nguo, akawa anahoji siku atakapokuwa hayupo nani atasimamia biashara zake kwani mumewe naye ni mfanyabiashara kwa hiyo yupo bize.
“Nilimuuliza anataka kwenda wapi hadi anasema hivyo, akajibu amewaza tu. Kumbe mawazo yake ni kama alijua dakika chache mbele ataiaga dunia.
“Sisi tuliokuwa tunatumia lifti tulipofika vyumbani mwetu tulijua yupo nyuma yetu. Kishindo kikubwa cha kitu kizito kuanguka ndicho kilichotushtua lakini hatukutoka nje.
“Baadaye ndiyo tukaletewa habari kwamba mwenzetu mama kichanga alianguka na kufa. Tulishtuka sana, tulilia kwani marehemu alikuwa mchangamfu kwa kila mtu ingawa siku ya kifo kama alipooza au kukosa raha. Kuna mwenzetu mmoja alimuuliza mbona leo huna raha, akasema anawaza maisha yake ya mbele,” alisema mwanamke huyo.

ALIJIRUSHA AU ALIANGUKA?
Mwanamke huyo alipoulizwa kama marehemu alijirusha mwenyewe, alirushwa au alianguka kwa bahati mbaya, alijibu:
“Hatujui. Hata manesi wenyewe walisema walimkuta amekufa chini, kwa hiyo hawajui kama alianguka au alijirusha kwa kuwa hakuna aliyemuona.”
MUME WA MAREHEMU NAYE
Akizungumza kwa uchungu kwenye msiba wa mkewe, Sinza - Mori jijini Dar, mume wa marehemu Lewina aitwaye Mashaka Mkude alisema:
“Kifo cha mke wangu mimi najua kilitokana na uchovu wa kupanda na kushuka kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya pili kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto.
“Mke wangu akiwa mjamzito alifika Muhimbili akiwa mzima wa afya, akajifungua mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji.
“Baada ya kujifungua, hali ya kichanga ikiwa si nzuri kiafya, alionekana ana manjano, yaani hali ya kubadilikabadilika na akalazimika kutengwa yeye na mtoto wake.
“Kutoka na hali hiyo mke wangu alishauriwa na daktari awe anakwenda kumnyonyesha mtoto kila baada ya saa tatu.
“Ilikuwa usiku wa saa sita kasoro, siku ya Jumanne, yeye na wenzake walipoamka kwenda kunyonyesha inadaiwa hakupanda lifti kama wenzake.
“Wakati wa kurudi inadaiwa kuwa marehemu alikuwa na mwenzake wakati wa kushuka, akashauriwa atumie lifti lakini alikataa.
“Baada ya muda mfupi wenzake walisikia kishindo kikubwa kumbe ni mke wangu alianguka kutoka juu na kufariki dunia palepale.
“Nina imani mke wangu alikuwa katika utaratibu wa kutimiza ushauri wa dakrari wake hali iliyompata ilitokana na uchovu wa kupanda ngazi na kushuka,” alisema mwanaume huyo.
Mashaka alikanusha vikali kuwa mke wake alijirusha na kumsababishia kifo, akisema marehemu hakuwa na tatizo lolote la kifamilia wala kiafya.
AZIKWA, KICHANGA BADO HOSPITALI
Habari zinasema kichanga hicho walichokipa jina la Biligita Mashaka kinaendelea vizuri katika uangalizi maalum hospitalini hapo ambapo kinawaliza wengi kutokana na masaibu yaliyotokea.
Marehemu alizikwa Ijumaa ya wiki iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

KAMANDA WA POLISI ILALA ATHIBITISHA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Komba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema marehemu alikutwa chini amekufa baada ya kuanguka kutoka kwenye ngazi za ghorofani.
KATIKA hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amenaswa akiwa ametinga khanga moja na kuwaacha watu midomo wazi.
Kajala alinaswa na kamera yetu maeneo ya Kigogo jijini Dar ambapo watu kibao walionekana kumzunguka na kuhoji kulikoni staa huyo ambaye amezoeleka kutika pamba kali, aonekane na vazi la khanga?
Akizungumza na Weekly Star Exclusive, Kajala alisema alilazimika kutinga khanga hiyo kuendana na matakwa ya filamu yaliyomtaka kuvaa vazi hilo na kuonesha mazingira ya uswahilini hivyo watu waliomzunguka walikuwa hawajui nini kinaendelea.
“Nilipoambia naigiza sinema ya Kigodoro nilishtuka sana lakini mwisho wa siku nilikubali kwa kuwa mimi ni msanii naweza kubadilika kivyovyote na nina imani mashabiki wangu wataniona kivingine, humo ni full mcharuko,” alisema Kajala.

Friday, October 18, 2013

Msanii anayeng’ara kwenye filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ juzikati aliwaacha midomo wazi watu baada ya kwenda kuchukua msosi mara tatu kwenye shughuli iliyochukua nafasi ndani ya Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar.
Lulu alikuwa kati ya wasanii waliofika eneo hilo kushiriki katika harambee ya kansa ya wanawake iliyoendeshwa na taasisi ya kuzuia kansa nchini ambapo baada ya zoezi hilo, waalikwa walijongea eneo la maakuli.
Huku akionekana mwenye ‘ubao’, Lulu alikwenda kwenye foleni na kuchukua pleti ya kwanza, akaifuta kisha akanyanyuka na kwenda kuchukua nyingine, nayo akaimaliza, baada ya muda akaenda kuchukua nyingine ambapo haikufahamika kama nayo aliifuta au alisaidiwa na mtu.
Akilizungumzia tukio hilo, Lulu aliliambia Ijumaa: “Nakula sana na hii ni kawaida yangu, najua watasema lakini kwenye msosi huwa sikai nyuma.”
KITENDO cha Mahakama ya Rufaa kukubali kusikiliza marejeo ya hukumu ya kifungo cha maisha jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kimetafsiriwa kuwa ni kama wamepata nafasi ya mwisho ya kuweza kujinasua.
WARAKA WA PAPII KOCHA
Mahakama hiyo ilikubali ombi hilo hivi karibuni na kueleza kuwa marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Papii Kocha kutuma waraka wa kuomba msamaha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ndiye aliyekubali kuufikisha kwa JK hivyo kuna madai kuwa huenda waraka huo ndiyo umezaa matunda.

WARAKA UMEZAA MATUNDA?
“Unajua ule waraka ulikuwa na maneno ya kuumiza sana. Inawezekana kabisa kuwa ulimfikia JK akaagiza suala hilo liangaliwe upya. Haina maana kuwa JK anaingilia sheria. Nadhani wanasheria wana vipengele vingi ambavyo vinaruhusu marejeo ya rufaa hiyo. Kilichopo hapa ni namna ya kuzitafsiri sheria kisha kuona kama rufaa hiyo inaweza kusikilizwa.
“Ninachojua ni kwamba Babu Seya na Papii Kocha wamepata nafasi ya mwisho ya kuweza kujinasua kwa sababu hata wakili wao (Mabere Marando) yupo vizuri katika kuwatetea wateja wake.
MUNGU ANAWEZA
“Mimi naamini Mungu anaweza yote hivyo tuwaombee rufaa yao iende vizuri,” alisema mmoja wa ndugu wa familia ya Nguza.
Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi iliyowahusisha na ubakaji wa watoto kumi wa Shule ya Msingi, Mashujaa iliyopo Sinza, Dar, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.

JOPO LA MAJAJI
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati.
Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010, mahakama hiyo iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza.

WATIWA HATIANI
Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, iliwatia hatiani Babu Seya na wanaye hao kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti.
Januari 27, mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25, mwaka 2004.
Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo kati ya Aprili na Oktoba 2003.
Wadau na mashabiki wa mastaa wawili nchini, Wema Sepetu wa Bongo Movie na Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa muziki wa kizazi kipya, wamebariki ndoa ya wapenzi hao kwa kusema kuwa ni watu wanaoendana na kutegemeana kwa kiasi kikubwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Wema na Diamond walitupia katika kurasa zao za mitandao ya kijamii picha zao, ambazo zinaonekana zilipigwa eneo moja kwa simu moja na hivyo kuwapa wakati mzuri mashabiki wao ambao walionekana kupendezwa na uhusiano wao na kupendekeza waoane.
“Hii ndiyo couple bomba zaidi ya wasanii Bongo, kwa nini msioane? Mnapendeza sana jamani, ebu Diamond Platnumz achana na Penny bwana, huendani naye kwanza kuna mambo ya dini na nini…,” aliandika shabiki mmoja.
Mwingine aliandika: “Nadhani Penny angejiweka tu pembeni awaache hawa wawili, ni mastaa kwa fani zao, yeye angeendelea tu na kazi yake ya utangazaji. Kwanza kwake ni maumivu tu kuwa na msanii ambaye ana shughuli nyingi za kisanii, bora wale wenyewe wanajuana.”
Ingawa kwa muda mrefu Diamond amekuwa akikanusha kurudiana na Wema, hivi karibuni picha zao zilivuja katika mitandao ya kijamii wakiwa China wakila bata na alipoulizwa, ‘alizuga’ eti walikuwa wakitengeneza filamu.
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, wadau wengi wanaamini Wema na Diamond wanapendana kwa dhati hivyo wakapendekeza wafunge ndoa na kuyaacha maisha mengine yaendelee kuwepo kuliko kuachana kisha kurudiana mara kwa mara.

Thursday, October 17, 2013

SASA ni saa tu zimeanza kuhesabika kabla ya mabingwa Yanga kushuka dimbani kukipiga na watani wao, Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, keshokutwa Jumapili.
Yanga SC.

Iwapo Simba ambao ni wenyeji watapoteza, itakuwa ‘noma sana’, maana watakuwa wameshindwa kulipa kisasi cha msimu uliopita, lakini Yanga pia ikifungwa, itakuwa ‘noma sana’, maana itazidiwa pointi sita na watani wake hao, si chache.
Mengi yanayozungumzwa kuelekea mchezo huo, kikubwa ni tambo za mashabiki wa kila upande ambapo wale wa Simba wanaamini Amissi Tambwe lazima awalize Wanajangwani hao, ambao nao wanaamini lazima Mrisho Ngassa awanyamazishe Msimbazi kama alivyoahidi.
Simba SC.

Tambwe atishiwa kuuawa
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum, Tambwe ambaye anaongoza kwa mabao katika ligi hiyo akiwa amefunga nane, amesema amekuwa akipigiwa simu kutoka kwa watu asiowajua wakimwambia ole wake aifunge Yanga, atakiona cha moto.
“Nimeshangaa sana hapa Tanzania watu wanavyoishi, nimekuwa nikipokea simu hizo mara kwa mara na wote wakinitishia kuniua kama nitaifunga Yanga, ukiwauliza wanasema tena kifo changu kitatokana na risasi, kama nataka usalama wangu basi nihakikishe siwafungi Yanga,” alisema Tambwe na kuongeza:
“Nimeshindwa kuwatambua kwa kuwa namba zao hazionekani (private number) kwenye simu yangu, wanaweza kuona kama nitaogopa vitisho hivyo, lakini nakwambia hali hiyo haiwezi kunizuia kufanya kazi yangu, nikipata nafasi nitafunga kama kawaida yangu, hii ndiyo kazi yangu.”

Tambwe amshangaa Ngassa
“Lakini kufunga ni mipango ya Mungu, nimesoma gazeti moja (Championi), nikaona mtu ameongea kitu cha ajabu kidogo, ni vizuri kujiwekea malengo lakini siyo kusema eti nisipofunga nitachoma moto nyumba zangu, nadhani hakutakiwa kutamka maneno hayo, amekosea sana,” alisema Tambwe.
Kauli hiyo ya Tambwe inakuja kufuatia Ngassa, kutamka kuwa atahakikisha anawafunga Simba au kutoa pasi itakayozalisha bao na kama atashindwa kufanya hivyo katika mechi hiyo, yupo radhi kuchoma moto nyumba zake tano zilizopo Dar na Mwanza.
Ngassa anawaza kufunga tu
Akizungumzia mechi hiyo, Ngassa alisema hana mawazo ya kuwa mfungaji bora lakini nia yake ni kuhakikisha Yanga inaibuka na ubingwa msimu huu huku yeye akifanya kazi yake inavyotakiwa.
“Akili na malengo yangu hivi sasa ni kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa, ninachotaka ni kufanya suala la ufungaji linakuwa lazima kwangu katika mechi zote na kama sitafunga basi nitoe pasi ya bao,” alisema Ngassa.

Maoni ya makocha
Kocha Hemed Morocco aliyemaliza mkataba wake na Coastal Union, amesema: “Ninaipa asilimia tisini Yanga kwa sababu ina muda kidogo ipo na wachezaji walewale, Simba bado inajipanga,” alisema Morocco.
Kuhusu mwamuzi wa mechi hiyo, Israel Nkongo, Mwenyekiti wa Matawi wa Vijana wa Yanga, Bakili Makele alisema: “Tunampa onyo na kumtaka mwamuzi kuchezesha kwa kufuata kanuni zote kumi na saba za soka, maana wapinzani wetu wamekuwa wakifunga mabao mengi kwa njia ya penalti, wanapata penalti zisizo za msingi.”
Upande wa Simba, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alipozungumza na gazeti hili alisema: “Tunampongeza mwamuzi kupata nafasi ya kuchezesha mechi hiyo lakini tunamtaka ahakikishe anafuata sheria zote za soka, mechi hii inaweza kumjenga au kumbomoa.”
Didier Kavumbagu.

Wilbert Molandi na Lucy Mgina
MSHAMBULIAJI wa Burundi, Didier Kavumbagu, amesema kuwa akiwa ndani ya uwanja katika mechi ya Ligi Kuu Bara keshokutwa Jumapili, ataweka undugu pembeni na beki wa kati wa Simba, Kaze Gilbert ambaye ni Mrundi mwenzake.
Kaze Gilbert.

Wachezaji hao wanaotoka nchi moja ya Burundi na waliowahi kucheza katika timu ya Vital’O inayoshiriki Ligi Kuu ya Burundi, watakutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza tangu waanze kuzitumikia klabu zao za hapa nchini.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kavumbagu alisema kuwa siku hiyo atakuwa kazini, hivyo suala la kuwa wametoka nchi moja ataliweka pembeni kwa muda.
“Mimi na Kaze ni kama ndugu kutokana na wote kutoka nchi moja, pia tumetoka wote kwenye klabu moja ya Vital’O ya Burundi, lakini katika mechi ya Simba na Yanga, undugu nitauweka pembeni.
“Yeye kama beki atafanya kazi yake ya kuzuia na mimi nitafanya kazi yangu ya kufunga,” alisema Kavumbagu.
Kocha wa Azam FC, Stewart Hall.

Na Khatimu Naheka
KOCHA wa Azam FC, Stewart Hall amezichambua Simba na Yanga, lakini akaeleza sababu mbili zitakazokinufaisha kikosi cha Yanga katika mchezo baina ya timu hizo keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Stewart ameliambia gazeti hili kuwa vikosi vya Simba na Yanga vina tofauti kubwa, ambapo Wekundu hao bado hawajafanikiwa kucheza vema, jambao ambalo vinaweza kuwapa wakati mgumu katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.
“Timu zote ni nzuri, lakini Simba naiona kama mpya yenye vijana wengi na kocha mpya, mpaka sasa bado hawajaweza kufikia ubora ule unaotegemewa na wengi,” alisema Stewart.
STAA wa sinema za Kibongo, Ummy Wenceslaus 'Dokii' amewakemea watu wanaomsema kuwa anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete na kuwataka waache kwani yeye hajipendekezi.
Ummy Wenceslaus 'Dokii'.

Akizungumza na Kipindi cha Action & Cut cha Channel Ten hivi karibuni, Dokii alisema kutokana na jinsi alivyoshiriki katika kampeni mbalimbali za Kikwete hadi kupata ajali na kuumia mkono, wambeya wamekuwa wakimzushia kuwa alijipendekeza na hakupewa msaada wowote alipoumia.
“Nawashangaa wanaosema kuwa najipendekeza kwa JK, eti wanasema nilitelekezwa. Kwa taarifa yao tu ni kwamba, JK aliposikia nimepata ajali, alituma madaktari Wazungu kuja kunihudumia.
“Halafu hata wakisema najipendekeza pia naweza nikakubali, nisipojipendekeza kwake wanataka nikajipendekeze kwa nani? Najua hata wao wanatamani kuwa karibu na viongozi kama mimi,” alisema Dokii.
MCHEZO mzima wa namna wahamiaji haramu 16 raia wa Somalia na Ethiopia waliokamatwa Jumamosi iliyopita mjini hapa umegundulika.
Watu hao walikamatwa wakiwa hoi baada ya kukosa hewa katika barabara kuu iendayo Iringa jirani na baa maarufu ya Mzuwanda, baada ya raia wema kuwapenyezea siri maofisa uhamiaji waliokuwa eneo la Msamvu.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinasema kwamba, lori hilo lenye namba za usajili T 707 CGY lilikuwa likitokea Ulolo, Tanga likielekea nchi za Zambia na Afika Kusini.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Godrfey Chambo aliliambia Amani kuwa, akiwa Msamvu na rafiki zake, walishangaa kuona mtu mwenye asili ya Somalia akidondoka kwenye lori ndipo walipoamua kufuatilia na kutoa taarifa kwa maofisa wa uhamiaji.
“Sisi tulikuwa na mishe zetu pale Msamvu, mara nikashangaa mtu anadondoka akiwa hoi, amechafuka na kitu kama unga, kumbe ni chokaa. Lile gari lilikuwa linajaza mafuta pale. Nikamwambia mwenzangu ndipo tukaamua kutoa taarifa kwa maofisa wa uhamiaji.
“Dereva alionekana kushtukia mchezo, alipomaliza kujaza mafuta, akaliondoa gari kwa kasi. Watu wa bodaboda wakaanza kulifukuza hadi walipokamatwa kule Mzuwanda,” alisema Chambo.
Jeshi la polisi mjini hapa kwa kushirikiana na watu wa uhamiaji baada ya kukamata gari hilo walikwenda nalo hadi Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa na kuwatoa wahamiaji hao ambapo wengine walifikishwa hospitalini kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Mmoja wa maofisa wa uhamiaji mkoa wa Morogoro, Wilfred Minja, alithibitisha kukamatwa kwa watu hao ambapo pia aliwashukuru raia wema kwa ushirikiano walioutoa wenye lengo la kulinda usalama wa nchi yetu.
MTOTO aitwaye Mwajuma Haji (16) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anayesumbuliwa na ugonjwa wa kusinyaa kwa viungo yuko katika hali mbaya baada ya baadhi ya ndugu kudaiwa kutaka auawe ili kutoa uchuro katika familia.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo, Tatu Musa baadhi ya ndugu (siyo wote) wamekata tamaa ya kumuuguza mtoto huyo na kupendekeza heri mtoto huyo akatishwe maisha yake.
“Mwanangu haumwi wala hajawahi kuumwa ila ghafla alianza kusinyaa na kukosa nguvu, kinachoniuma baadhi ya ndugu zangu wamekata tamaa wanataka wamuue, waniachie mwanangu,” alisema mama huyo huku akilia mfululizo.
Mwandishi wetu amemshudia mtoto huyo akiwa amesinyaa viungo kiasi cha kutoweza kufanya kitu chochote zaidi ya kulala.
Mama mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa alijifungua mtoto huyo akiwa na afya njema lakini alipofikisha umri wa miaka mitatu hali ikabadilika na viungo vyake kuanza kusinyaa.
Mama huyo amedai kwamba kutokana na hali hiyo hakuweza tena kufanya shuguli za kumwingizia kipato zaidi ya kukaa na mwanaye kijijini kwao, Kiamange, Bagamayo mkoani Pwani bila ya kupata matibabu ya uhakika.
Alisema kwamba maisha ya mtoto wake yameendelea kuwa mabaya bila ya kupata msaidizi kutokana kutengwa na baadhi ya ndugu zake waliokata tamaa ya kumuuguza.
Aidha, Mama Mwajuma amedai kwamba kuna wakati alikuwa akimfungia ndani mwanaye kuanzia asubuhi ili aende kulima na kupata chochote, lakini aliporudi nyumbani alimkuta katika hali mbaya sana.
Kutokana na mazingira kuwa magumu, mama huyo alidai kwamba hakuwa na msaidizi wa kuweza kumwachia mwanaye ili aweze kuhangaikia kipato.
Mbali na mtoto huyo, mama huyo alibahatika kupata mtoto mwingine ambaye sasa ana umri wa mwaka mmoja na nusu lakini baada ya kujifungua mwanaye mkubwa akatokwa na vidonda mgongoni.
Baada ya mtoto huyo kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu alishauriwa kumpeleka Muhimbili na kumuacha mwanaye mdogo kwa majirani.
Baada ya muda alipata taarifa kwamba mtoto wake mdogo anaumwa, ikabidi akamchukue na kumleta Muhimbili ili aishi naye ingawaje hairuhusiwi kwa mtoto kuishi wodini.
“Nina wakati mgumu, kwa kuwa nina watoto wawili sina cha kufanya kwa kuwa huyu mwingine hajiwezi kwa chochote zaidi ya kumsaidia kwa kila kitu, mbaya zaidi ndugu wamenitenga,” alisema huku akibubujikwa machozi.
Ndugu Mtanzania mama Mwajuma yuko katika hali mbaya sana, kama unataka kumsaidia mtoto wake tuma mchango wako kupitia namba 0754 021 3
STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekataa kabisa suala la kuolewa kwa sasa akidai moyo wake haupo tayari kwa tendo hilo.
\
Lulu alifunguka hayo Jumatatu iliyopita katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kupitia Runinga ya East Africa ambacho humpa nafasi staa kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu maisha yake na sanaa kwa jumla.
Wakati mahojiano hayo yakiendelea, mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho anayefahamika kwa jina la Muba, alimtupia Lulu swali ambalo lilimtaka aeleze utayari wake endapo mtu akijitokeza na kutaka kumuoa.
“Sitaki kuolewa kwa sasa, muda wa kuolewa haujafikia. Ukifika nitafanya hivyo lakini kwa sasa sipo tayari kuolewa,” alisema Lulu.
Aidha, Lulu alikiri kuwa licha ya kutokuwa tayari kuolewa lakini amekuwa akipata usumbufu mkubwa wa kutongozwa na wanaume. Aliainisha kuwa alikuwa akitongozwa kabla na baada ya kutoka Segerea alipokuwa akishikiliwa kwa kesi ya kifo cha aliyekuwa mpenzi wake, marehemu Steven Kanumba.
“Watu wananitongoza sana, walikuwa wakifanya hivyo kabla hata sijaingia China (gerezani Segerea) na wameendelea kufanya hivyo hata baada ya kutoka,” alisema Lulu na kuongeza:
“Siwezi kuwakubalia sababu sipo tayari kuolewa kwa sasa…muda wa kufanya hivyo haujafika.”
Kuhusu suala la kudaiwa kutembea na bosi wa Kampuni ya Proin Promotion ambayo inamsimamia kisanii kwa sasa, Lulu aliruka viunzi na kudai taasisi hiyo inamlea kama mtoto wa familia na siyo vinginevyo.
Alisema hata madai yanayoelekezwa kwake kuwa Proin wamempa gari na nyumba kama sehemu ya kuhongwa na bosi wa kampuni hiyo, hayana ukweli wowote kwani yeye anafanya kazi kama msanii chini ya kampuni hiyo na hakuna kitu cha ziada.
“Hahahaha! Salama (mtangazaji) acha mambo yako bwana… mimi nipo chini ya Proin kwa sasa kwa kipindi flani ambacho nimesaini nao mkataba. Wananilea kama msanii wao, hakuna cha ziada,” alisema Lulu.
Akiendelea kubwabwaja maneno ndani ya kipindi hicho, Lulu aliweka wazi kuwa alikuwa akishindwa kuanika penzi lake na marehemu Kanumba kwa kuwa muda muafaka ulikuwa haujafika na kudai waliishi kama mtu na baba yake kabla hawajawa wapenzi, wakawa wapenzi na mauti yakamkuta Kanumba kabla hawajalianika penzi lao.

Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawili Bongo, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ na Steven Kanumba ‘The Great’.
Mchungaji Mayanga (mwenye kipaza sauti) akitoa ushuhuda.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita ya Oktoba 13, mwaka huu, huko Mzambarauni, Mbagala-Charambe jijini Dar katika Kanisa la Powerful Gospel Ministry lilipo chini ya Mchungaji Meshak Punkanya ambapo Mayanga alipewa nafasi ya kutoa ushuhuda.

VIFO MILIONI 605
Mchungaji huyo alielezea kujuta kwake mbele ya kanisa kwa kudai kuwa kabla ya kuokoka alikuwa mchawi mkubwa aliyeishi kuzimu na kufanya kazi za mauaji sambamba na shetani mkuu (Lusifa) kwa kuwatumia vibaraka wake na majini.
Mchungaji Mayanga alikiri kutekeleza vifo vya watu wapatao milioni 605 wakiwemo waigizaji hao.
Steven Kanumba.

WAMO FIVE STARS, MTOTO WA DANDU
Alisema kuwa kati ya watu aliowaua kwa njia za kishirikina wamo waimbaji wa Taarab wa Kundi la Five Stars wapatao 14, Kanumba, Sharo Milionea na mwanamuziki James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’.
Pia alidai kuwa alihusika katika vita kati ya aliyekuwa Rais wa Iraq, Sadam Hussein na Marekani kwa kutumia pepo la uchonganishi alilolitaja kwa jina la ‘Magweju’.
Pia mchungaji huyo alidai kuhusika na shambulio la hivi karibuni la Al-Shabaab katika maduka ya Westgate la Nairobi nchini Kenya na matukio mengine mengi hadi kufikia idadi hiyo ya vifo vya watu milioni 605.
Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’.

AWAONEA HURUMA WASANII, AWAONYA
Mchungaji huyo aliendelea kusimulia kuwa alipokuwa katika ulimwengu wa giza aliwahi kuwaonea huruma wasanii kama Kanumba, Sharo Milionea na Mtoto wa Dandu na kuwatokea kimiujiza akiwaonya waokoke kabla ya kuchukua roho zao huku mashabiki wao wakibaki na simanzi wakiamini kuwa vifo vyao ni vya kawaida.
Alidai kuwa baada ya kuwafuata mastaa hao na kuwaonya walikataa na badala yake akawaua.
Akiendelea kulishuhudia kanisa, Mchungaji Mayanga alisema kuwa kwa sasa ameokoka na kuachana na mambo ya giza, hivyo haogopi kuzungumza ukweli kwa kuwa roho wa Bwana anamuongoza kushuhudia kila kitu alichokifanya ili waumini watambue uwezo wa Mungu.
Gari la Sharo baada ya ajali.

ANA SIRI NZITO ZA VIGOGO
Huku akiomba hifadhi ya majina ya wahusika, mchungaji huyo alihitimisha ushuhuda wake kwa kudai kuwa ana siri nzito za vigogo au watu wakubwa ambao aliwahi kwa namna moja au nyingine kuwapa utajiri wa nguvu za giza.

UTABIRI
Hata hivyo, baadaye jamaa huyo alijitabiria kuwa atakamatwa na kufungwa siku moja kutokana na siri alizonazo.
“Yaani nina siri za watu wengi sana, nikiwaambia mtaogopa na nchi itatikisika. Najua siku moja watu watanikamata na kunifunga pingu kwa siri nilizonazo, lakini kamwe siogopi kwa kuwa Bwana ananiongoza,” alisema Mchungaji Mayanga.
Jeneza la Kanumba.

KANUMBA, SHARO MILIONEA
Kanumba alifariki dunia mwaka jana akiwa nyumbani kwake Sinza-Vatican, Dar huku Sharo Milionea akipoteza uhai kwenye ajali ya gari iliyotokea wilayani Muheza, Tanga wakati msanii huyo akienda kwao mkoani humo akitokea Dar.

Other blogs

Copyright ©2013 Gabriel Fredy . Powered by Blogger.

Total Pageviews

GABRIEL FREDY

SELECT LANGUAGE

DIEGO COSTA'S GOAL ON CHELSEA

Popular Posts